Jumanne 26 Agosti 2025 - 00:34
Wanazuoni wa Sunni wa Lebanon Wameunga Mkono Muqawama kikamilifu

Hawza / Sheikh Ahmed Al-Qattan, kiongozi wa dini wa Sunni na Rais wa Jumuiya ya “Qoulna wa Al-Amal” nchini Lebanon, amesema: “Tunasema kwamba silaha zilizopo Lebanon na sehemu yoyote ambapo silaha zipo kwa ajili ya kuilinda nchi, watu, na sehemu takatifu, kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu, ni marufuku kuzitoa upande wowote ambao huenda usingeweza kulinda

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmed Al-Qattan alionyesha kushangazwa kwake kisiasa kuhusu uwasilishaji wa mfungwa mmoja wa Kizayuni ndani ya Lebanon kwa maadui wa Kizayuni na Serikali ya Lebanon.

Alisema: “Sote tunajua kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wasio wa kijeshi wa Kilebanoni ambao wako mikononi mwa maadui wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizoko chini ya wakoloni, Je, nchi yetu inaweza kukubali kumkabidhi Mzayuni mmoja kwa maadui bila fidia yoyote? Fidia hii angalau ingehitaji kurudishwa kwa baadhi ya raia wasio wa kijeshi waliokuwa wafungwa katika magereza ya maadui wa Kizayuni.”

Sheikh Al-Qattan aliongeza: “Hichi ndicho hasa kile ambacho serikali na nchi zinazozungumza kuhusu amani na uhusian wa kawaida na maadui hawa wanataka, wanataka kutoa kila kitu lakini hawataki kupokea chochote kutoka kwa maadui hao, wala hawaruhusiwi kupokea chochote.”

Aliongeza zaidi: “Kwa hivyo, tunasema kwamba silaha zinazopo Lebanon na sehemu yoyote ambapo silaha zipo kwa ajili ya kulinda nchi, watu, na sehemu takatifu, kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu, ni marufuku kuzitoa upande wowote ambao huenda usingeweza kulinda.”

Kiongozi huyu wa dini ya Sunni alifafanua kuwa: “Hii ndiyo imani yetu na hii ni fatwa ya kidini, kulingana na Sheria ya Kiislamu, si halali kuwasilisha nguvu zetu kwa namna ambayo maadui wanaweza kuzikomboa na kutushambulia, hatujatoa kile kilichobaki cha nguvu zetu, na tunashuhudia mashambulizi ya kila siku ya mauaji, uharibifu, na ukoloni ambao bado unaenea katika ardhi zetu, tunashuhudia ukiukaji wa kila siku wa uhuru wa nchi yetu  unataka tuchukue hatua ya kuzipa silaha zetu ili maadui waweze kuendelea na ukatili, wauwe wote, na kuchukua udhibiti na ukoloni wa ardhi yetu yote.”

Aliongeza kuwa: “Ni nani kati yetu anaweza kuwadhamini maadui? Ni kundi gani ndani ya Lebanon au sehemu nyingine? Ni nani anaweza kutoa dhamana? Ikiwa Marekani inasema siwezi kutoa dhamana, ni nani atakayethibitisha kwamba maadui hawa wa Kizayuni hawaingii Lebanon na kuchukua kuidhiti, kama walivyofanya katika maeneo matano na kama wanavyoshambulia ardhi na nchi yetu kila siku?”

Sheikh Ahmed Al-Qattan alisema: “Tuwe waangalifu na wa busara, tukajiweka katika kundi la wale wanaowajibika kulinda nchi yetu na nguvu zinazolinda, tuna imani na jeshi la Lebanon kuwa kubwa na lenye nguvu, na inshaAllah jeshi halitahusishwa katika vita vya ndani au migogoro na watu na taifa letu, kwa sababu tuna uhakika kwamba jeshi ni mlango wa usalama na alama ya amani ya kiraia nchini Lebanon, kwa hivyo, tunamuomba Mwenyezi Mungu ailinde nchi yetu, Lebanon, na pia nchi zote za Kiarabu na Kiislamu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha